Huwezi kusikiliza tena

DRC yakataa msaada wa MONUSCO

Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo imakataa msaada wowote kutoka kwa vikosi vya umoja wa mataifa MONUSCO katika operesheni dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR.

Rais Joseph Kabila , alitoa kauli hiyo hapo jana katika hotuba kwa mabalozi mjini Kinshasa.

Msemaji wa serikali ya Kongo, Lambert Mende, alisema kuwa hio ilitokana na utata uliopo katika mawasiliano ya pande hizo mbili.

MBELECHI MSOSHI ametutumia taarifa ifuatayo kutoka Kinshasa.