Huwezi kusikiliza tena

Wauza Miraa wamegoma kuipeleka Somalia

Wafanya biashara wa marungi au miraa wa Kenya, wameacha kusafirisha bidhaa hiyo kwenda Somalia kwa sababu imekuwa ghali mno.

Waraibu wengi wa vikonyo hivyo vya miraa wako Somalia.

Mfanyi biashara mmoja ameiambia BBC kuwa wakulima wa miraa wamezidisha bei yao maradufu, hadi kufikia dola mia 6 kwa gunia, na serikali ya Somalia imepandisha ushuru hadi dola mia mbili kila gunia.

Kulikuwa na safari 16 za ndege kusafirisha miraa kutoka Kenya hadi Somalia kila siku, zote zimesimama.

Sehemu nyingi za Somalia zinategemea miraa kutoka Kenya, kwa vile hailimwi Somalia, ambako inapendwa sana.

Wakulima wa miraa wa Kenya waliumia pale serikali ya Uingereza, ilipopiga marufuku miraa kuingizwa nchini.