Huwezi kusikiliza tena

Kesi ya Rugulika yahairishwa Burundi

Nchini Burundi kesi inayomkabili Mwandishi wa Habari Bob RUGURIKA imeahirishwa baada ya kusikilizwa jana katika Mahakama ya Rufaa ya Bujumbura.

Mtuhumiwa huyo ambae pia ni Mkurugenzi wa redio maarufu nchini humo ya RPA anatuhumiwa kupanga njama na wahalifu baada ya kumuhoji redioni mtu aliyedai kuhusika na mauaji ya watawa watatu wakiitaliano mwaka jana kwa amri ya idara ya ujasusi.

Amekana tuhuma zinazomkabili.