miradi ya nishati yaanzishwa barani Afrika kupunguza ufukara
Huwezi kusikiliza tena

Miradi ya kuzalisha nishati yaanzishwa

Gharama ya nishati barani Afrika inakisiwa kuwa ghali zaidi kuliko mabara mengine duniani, hali inayofanya gharama ya maisha kupanda kwa kiasi kikubwa katika mataifa yote yanayostawi.

Hali hii imesababisha viwango vya umasikini kuongezeka na hivyo mataifa mengi hulazimika kutegemea misaada kutoka kwa mataifa ya nje, kukidhi mahitaji yake.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni bara la Afrika limeibuka kuwa bara ambalo linaelekea kutumia zaidi nishati safi na isiyochafua mazingira.

Miradi kadhaa ya kuzalisha nishati kupitia miale ya jua imeanzishwa barani humo.

Mwandishi wetu Robert Kiptoo alizuru eneo la kaskazini mwa kenya na kutuandalia ripoti ifuatayo.