Viajana waingilia muziki Tanzania ili kukimu maisha
Huwezi kusikiliza tena

Vijana waingilia muziki TZ kukimu maisha

Muziki nchini Tanzania umekuwa kimbilio la vijana wengi ikiwa ni moja ya njia za kujikwamua dhidi ya umaskini kutokana na ukosefu wa ajira.

Vijana hao wanaenda mbali zaidi kiasi huku baadhi yao wakiwa tegemeo la familia zao.

Kutoka Dar es salaam, Arnold Kayanda anaongea na Dogo Aslay kijana mdogo anayewatunza wazazi kutokana na uimbaji wake katika YA MOTO BAND inayoundwa na vijana wadogo, wengi wao wakiwa katika umri wa miaka ishirini hivi.