Huwezi kusikiliza tena

Mbwa kitoweo murua China

Baadhi ya wachina waishio Tanzania hapo jana waliungana na wenzao duniani kuadhimisha mwaka mpya wa kichina.

Hata hivyo wakati wachina hao wakiadhimisha mwaka huo baadhi ya raia wa Tanzania wamekuwa wakistaajabu vyakula wanavyokula wachina kwani kwa upande wao haviliwi.

Miongoni mwa vyakula vinavyofurahiwa wakati wa sherehe hizi ni pamoja na nyama ya mbwa.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Arnold Kayanda amezungumza na Profesa Jang Shao Jin mchina ambaye kwake haoni tatizo kula nyama ya mbwa.