Huwezi kusikiliza tena

Rais wa Tanzania ndio mwenyekiti wa EAC

Viongozi wa mataifa matano wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki wamekutana katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Katika kikao cha leo Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alipokezwa uenyekiti wa Jumuiya hiyo baada ya Uhuru Kenyatta wa Kenya .

Miongoni mwa mambo yaliojadiliwa ni mataifa ya Somali na Sudan Kusini ambayo yatasubiri kwa mda mrefu kwa wao kujiunga na jamii hiyo.

Vilevile mpango wa kuunda serikali ya Shirikisho la Afrika mashariki ulijadiliwa.

Nchi wanachama zinatarajiwa kuwateua wataalamu kuanza kuunda katiba ili kuidhinishwa kwa serikali hiyo .