Baadhi ya watu wakitoka katika eneo la Mafuriko
Huwezi kusikiliza tena

Watu 38 wafa kwa mafuriko Tanzania

Watu 38 wanaripotiwa kufa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania katika mkoa wa Shinyanga kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia March tatu ikiambatana na upepo mkali.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga ameiambia BBC kuwa baadhi ya waliokufa ni kutokana na kuangukiwa na nyumba na miti kutokana na mafuriko hayo.

Mwandishi wa BBC Leonard Mubali amezungumza na Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha