Mtoto mwingine Albino akatwa mkono
Huwezi kusikiliza tena

Mtoto mwingine Albino akatwa mkono

Matukio ya mauaji na ukataji viungo vya albino yanaendelea kuwa tishio nchini Tanzania baada ya mtoto mwenye umri wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono,

katika shambulio jipya lililotokea mkoa wa Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Mtoto huyo kiume Baraka Cosmas alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.

Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino.

Na muda mfupi baada ya Rais Tanzania Jakaya Kikwete kukemea mauaji ya albino, ambao viungo vyao hutumika katika shughuli za kishirikina kwa imani potofu kuwa zinasaidia kuleta utajiri na madaraka.

Mwandishi wa BBC wa Dar es Salaam Regina Mziwanda alizungumza na Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda