Kitendawili cha Mohammed Emwazi, kijana aliyekuja kujulikana kama "Jihadi John" bado hakijateguliwa.
Huwezi kusikiliza tena

Kwanini kimya kuhusu Chinja Chinja wa IS

Kitendawili cha Mohammed Emwazi, kijana aliyekuja kujulikana kama "Jihadi John" bado hakijateguliwa.

Taarifa mpya sasa kutoka Tanzania zinasema alikataliwa kuingia nchini humo baada ya kuonekana amelewa na kufanya fujo uwanjani.

Emwazi, kutoka magharibi mwa London, ametambuliwa kuwa mpiganaji anayejifunika sura katika video kadhaa za kundi la linalojiita Islamic State ambapo amekuwa akiwakata vichwa mateka.

Mwandishi wetu Tulanana Bohela amezungumza na Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Mathias Chikawe kuhusu suala hilo.