Huwezi kusikiliza tena

Mamia ya watoto watoweka Nigeria

Maelfu ya watoto wanadaiwa kutoweka kutoka katika mji wa Damasak, kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Awali mji huo ulikuwa ukishikiliwa na wapiganaji wa Boko Haram.

Mwanamume mmoja aliiambia BBC kwamba anaamini kuwa watoto wapatao mia tano wametoweka, lakini huu si ushahidi wa moja kwa moja kuthibitisha upotevu wa watoto hao.

Regina Mziwanda amezungumza na Mwandishi wa BBC, Salim Kikeke aliyeko Abuja, Nigeria na kwanza alitakaka kujua ukweli juu ya tukio hilo.