Polisi mwingine aua mtu mweusi, Marekani

Wakuu katika jimbo la South Carolina nchini Marekani wamemhukumu Afisa mmoja wa polisi mweupe, kwa kosa la mauaji.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumpiga risasi raia mmoja mweusi na kumuuwa.

Picha ya Video ya kilichofanyika imewekwa mtandaoni.

Mkanda huo wa video unaonesha mtu mmoja kwa jina, Walter Scott, akipigwa risasi alipokuwa akimkimbia afisa huyo.