Afisa wa polisi aliyempiga risasi mtu mweusi nchini Marekani ashtakiwa
Huwezi kusikiliza tena

Afisa aliyemuua mtu mweusi ashtakiwa US

Afisa mmoja mzungu katika jimbo la Karolina ya Kusini nchini Marekani ameshtakiwa kwa mauaji ya mtu mweusi, ambaye inaelekea ni dhahiri alikuwa akijaribu kukimbia Jumamosi iliyopita. Afisa huyo mzungu ameshtakiwa baada ya picha ya video kuonesha tukio hilo katika eneo la Charleston ya Kaskazini. Maandamano kadha yamefanyika nchini Marekani kupinga mauaji ya watu weusi wakiwa mikononi mwa polisi katika maeneo mbalimbali nchini Marekani. Alex Mureithi ana maelezo zaidi.