Serikali ya Kenya imeamuru kufungwa kwa kampuni za hawala ili kuzuia ufadhili wa makundi ya kigaidi
Huwezi kusikiliza tena

Kampuni 13 za hawala zafungwa Kenya

Serikali ya Kenya imeamuru kufungwa kwa kampuni kumi na tatu za kusafirisha na kupokea fedha ili kuzuia waislamu wenye msimamo mkali kutumia njia hiyo kufadhili mashambulio ya kigaidi.Waziri wa usalama wa ndani Kenya Joseph Nkaissery ameiambia BBC kuwa akaunti za benki themanini na sita zimesitishwa; zikiwemo zile zinazoaminika kuhusika na kampuni ya kisomali ya mabasi na hoteli. Hatua hii imekuja kufuatia shambulio kwenye chuo kikuu cha Garissa wiki iliyopita ambapo watu zaidi ya mia moja waliuawa na wapiganaji wa Al-shabab.Baadhi ya wananchi wa Kenya wamezungumzia hatua hii ya serikali.