Rashid Mberesero akiwa katika amzingira ya shule baada ya kuhitimu darasa la saba
Huwezi kusikiliza tena

Maswali ni mengi juu ya Rashid Mberesero

Wiki mbili baada shambulio la chuo kikuu cha Garissa, maswali bado yamebaki bila majibu kuhusu mmoja wa watuhumiwa raia wa Tanzania. Rashid Mberesero , aligundulika katika eneo la tukio akiwa sio mwanafunzi wala mfanyakazi wa chuo hicho. Je,huyu kijana ni nani na kwanini yuko mbali na nyumbani. Mwandishi wetu Tulanana Bohela amesafiri hadi mji wa Gonja, kaskazini mwa Tanzania alipokulia Mberesero pamoja na mji wa Dodoma alikokuwa akisoma, na kutuandalia ripoti ifuatayo.