Huwezi kusikiliza tena

Wawekezaji wa Kichina Tanzania

Uwekezaji wa Kichina nchini Tanzania wamelalamikiwa kwa hatua yao kufanya biashara za reja reja hali ambayo inadaiwa kuwanyima fursa zaidi wenyeji wasio na uwezo wa biashara kubwa.

Katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam si ajabu kukutana na baadhi ya wachina wakiwa na biashara mikononi kama wafanyabishara wadogo nchini humo maarufu kama machinga hali inayozua mshangao na viulizo kwamba kweli hawa ni wawekezaji ama wamegeuka kuwa wafanyabiashara ndogo ndogo. Nilitembelea eneo la kibiashara la Kariakoo ili kujionea hali halisi.