Huwezi kusikiliza tena

Muziki wa kizazi kipya Tanzania

Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania umeanza kujitengenezea njia mpya kwenye soko la muziki.

Hatua hiyo ni baada ya wasanii wengi wa muziki huo kuanza kutumia ala za muziki wakiwa majukwaani na kuweka kando matumizi ya CD au muziki uliotengenezwa wa teknolojia ya kompyuta.

Licha ya kurejesha historia ya muziki nchini Tanzania na kuuongezea thamani muziki huo maarufu kama Bongo fleva, Mabadiliko haya yaliyoanza kujitokeza katika siku za hivi karibuni, yanawavutia wapenzi wa muziki nchini humo.

Mwandishi wetu Faraja Sendegeya ametuandalia taarifa ifuatayo kutoka Dar Es Salaam.