Bondia wa zamani kutoka nchini Uganda Kassim Ouma amesema kuwa Mayweather atapigwa na Manny Pacquiao
Huwezi kusikiliza tena

Bondia wa zamani asema Mayweather atajuta

Mashabiki wa ndondi kote duniani wanasubiri kwa hamu pigano kubwa wikendi hii huko Las Vegas, Marekani, kati ya Floyd Mayweather wa Marekani kwa jina la utani ''Money Man'' na Manny Pacquiao wa Ufilipino kwa jina la utani ''Pacman''. Mayweather, ambaye hajashindwa kwa mapigano yake yote 47 ni bingwa wa dunia uzani wa welter chama cha WBC na WBA naye Pacman ni bingwa wa WBO, na ameshinda mapigano 57, akapoteza matano na akaenda sare mara 2. Zaidi ya dola milioni 200 zinapiganiwa, Mayweather akipokea asilimia 60 na Pacman asilimia 40, zikiwa ndizo fedha za juu zaidi kupiganiwa katika historia ya ndondi za kulipwa. Kuanzia leo hii tunawapa ripoti maalum kuhusu pigano hilo....John Nene amezungumza na bondia wa Uganda ambaye makao yake ni Marekani Kassim Ouma, na kutuandalia ripoti hii.