Huwezi kusikiliza tena

Uhalifu kukomeshwa Afrika kusini

Nchini Afrika ya Kusini wabunge wameambiwa kuwa operesheni kabambe inapangwa kupambana na vitendo vya kihalifu katika majimbo yote ya nchi. Hii ni sehemu ya mpango wa kuzuia visa vinavyojirudia vya ubaguzi kama vya hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Meja Jenerali Charl Annandale wa huduma ya Polisi amesema kuwa mashambulizi ya wageni yameanza kupungua. Anasema kuwa wabunge wamefahamishwa kuhusu idara 20 za serikali zinavyoshirikiana kuzuia na kuondoa uwezekano wa mashambulizi ya kiubaguzi yasirudiwe. Hassan Mhelela amekusanya maelezo haya kutoka Johannesburg.