Huwezi kusikiliza tena

Mahakama yakubali Nkurunziza agombee

Mahakama ya katiba ya Burundi imempa idhini rais Pierre Nkurunziza nafasi ya kuwania muhula wa tatu. Kabla ya tangazo hilo, naibu wa rais wa mahakama hiyo ameondoka Burundi, akielezea kwamba alichagizwa na hata kutishwa kuuawa ili aidhinishe hatua hiyo. Alidai kwamba wanne, kati ya majaji saba katika mahakama hiyo, awali waliamini msimamo huo wa rais sio halali, lakini wakalazimishwa kubadilisha nia. Lakini seneta wa chama tawala cha CNDD-FDD amekanusha madai hayo Wakati huohuo mamia ya waandamanaji waliingia katika barabara za Bujumbura wakiwa na hasira kufuatia umamuzi huu.Robert Kiptoo yuko mjini Bujumbura.