Umoja wa Mataifa unasema kuongezeka kwa  idadi ya wakimbizi kunatokana na ongezeko la mizozo
Huwezi kusikiliza tena

UN:Mizozo yaongeza idadi ya wakimbizi

Kila siku watu takriban elfu thelathini wanatoroka makwao wakikimbia vita na vurugu. Umoja wa Mataifa unasema idadi hiyo imetokana na ongezeko la mizozo hasa katika mataifa manne - Syria, Iraq, Ukraine, na Sudan Kusini. Mkataba wa amani Sudan Kusini haujatekelezwa huku maelfu wakiendelea kuumia. Mwandishi wetu Emmanuel Igunza ametembelea kambi moja ya wakimbizi kwenye jimbo la Jonglei na kuona hali ilivyo.