Kutokana na ghasia nchini  Burundi,inakadiriwa  karibu raia wa Burundi elfu ishirini wamevuka kuingia nchi jirani ya Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Ghasia Burundi:Raia wakimbilia Tanzania

Kutokana na ghasia katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, inakadiriwa kuwa karibu raia wa Burundi elfu ishirini wanavuka mpaka kuingia nchi jirani ya Tanzania. Tayari idadi hiyo inawalemea wenyeji na mashirika ya misaada ya Kimataifa yanayojaribu kuwasaidia wanaotafuta hifadhi kuingia. Mwandishi wetu Tulanana Bohela amekuwa Kagunda, ambako raia wengine zaidi wanakuja, na ametutumia taarifa ifuatayo.