Marekani na muungano wa Ulaya wataka uchaguzi uahirishwe Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Nkurunziza azungumza kuhusu uchaguzi

Marekani na jumuiya ya Ulaya wote wameitisha kuahirishwa kw a uchaguzi wa Burundi kufuatia wiki kadhaa za ghasia zinazopinga uteuzi wa Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu. Wakati huo huo, Rais Pierre Nkurunziza alikuwa katika mji wake wa nyumbani kwenye mkoa wa Muyinga ambako amezindua kampeni ya chama chake cha CNDD huku uchaguzi wa ubunge na mitaa ukinukia. Hapo awali aliwahotubia waandishi habari.