Huwezi kusikiliza tena

Mzozo wa Sudani Kusini waathiri uchumi

Katika majumaa kadhaa yaliyopita, zaidi ya watu laki moja wamefurushwa katika majimbo ya Unity na Upper Nile nchini Sudani kusini kufuatia kuzuka upya kwa mapigano. Wataalam wa uchumi wanaonya kuwa mzozo huo umeathiri pakubwa uchumi wa Sudan Kusini, na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola. Ripoti mpya inayoangazia athari hiyo inasema kuwa mapigano hayo ya zaidi ya miezi kumi na saba sasa, yameigharimu Sudan Kusini zaidi ya dola bilioni hamsini huku mataifa jirani na jamii ya kimataifa ikikadiriwa kutumia zaidi ya dola bilioni mia moja iwapo mzozo huo utaendelea kwa miaka mitano zaidi. Mwandishi wetu Emmanuel Igunza na mengi zaidi.