Huwezi kusikiliza tena

Burundi itaahirisha uchaguzi?

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amekuwa kimya kuhusiana na pendekezo linalotolewa na viongozi mbalimbali duniani kumtaka kuahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Miongoni mwa viongozi wanaopendekeza kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana na hali ya vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini Burundi ni pamoja na Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini, Umoja wa Ulaya na wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki ambao wamepanga kukutana tena hivi karibuni kutathmini hali ya kisiasa nchini humo.

Mwandishi wetu Leonard Mubali na taarifa zaidi