Shambulio jingine la Kigaidi Garissa
Huwezi kusikiliza tena

Al Shabab washambulia tena Garisa

Sasa imethibitishwa kwamba shambulio lililofanywa na wanamgambo wa Alshaabab katika kijiji cha Yumbis huko Garisa kaskazini mwa Kenya mapema jana limewajeruhi maafisa usalama kadhaa huku mmoja wao akipoteza uhai.

Awali kulikuwa na taarifa zinazokinzana baina ya serikali na vyombo vya habari nchini humo kuhusu idadi ya polisi walioathiriwa na mkasa huo .

Sasa serikali imeongeza idadi ya walinda usalama waliopelekwa eneo hilo huku ndege za kijeshi zikisaidia katika kuwasaka wapiganaji hao wa alshaabab -

Kuhusu hali ilivyo , awali Mwenzetu Jamhuri Mwavyombo alizungumza na diwani wa kata ya Yumbi huko Garrisa, Mahat Osman Ibrahim .