wachezaji wanaojipamba
Huwezi kusikiliza tena

Kocha akerwa na mapambo ya wachezaji

Kwa miaka ya hivi karibuni baadhi ya wachezaji wa kandanda wa Afrika Mashariki wameiga mitindo ya wachezaji wa ligi za Ulaya kama vile kupaka nywele zao rangi za kila aina, kwa mfano manjano,wengine nyeupe hadi katika ndevu zao na wengine nao wakivalia vipuli..Tabia hii imemkera sana kocha mzoefu wa timu ya Bandari ya Kenya, Twahir Muhiddin. Anawaomba waache tabia hii, na wawe jinsi walivyozaliwa. Akiwa mjini Mombasa John Nene amezungumza na Muhiddin.