Taasisi zinazokuza ugaidi kuchukuliwa hatua Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Serikali ya Tanzania yaonya kuhusu ugaidi

Nchini Tanzania Serikali imesema kuwa itazichukulia hatua kali taasisi ama kikundi chochote kitakachogundulika kujihusisha na kutoa mafunzo ya vitendo vinavyoashiria ugaidi au kuhatarisha amani kwa namna yoyote.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Dar-Es-Salaam Said Meck Sadiq,alipokuwa akizungumza na wanachama wa taasisi moja ya kiislam JUWAQUTA iliyotaka msimamo wa serikali baada ya watu wasiojulikana kukutwa katika madrasa moja mjini Morogoro inayomilikiwa na taasisi hiyo.

Mwandishi wetu Regina mziwanda kutoka Dar-Es-Salaam anaarifu zaidi.