Watu na Wanyama pori wasombwa Georgia
Huwezi kusikiliza tena

Watu na Wanyama pori wasombwa Georgia

Mafuriko makubwa yaliyoikumba mji mkuu wa Georgia, Tbilisi,yamesababisha maafa makubwa huku watu 8 wakithibitishwa kufariki.

Lakini hiyo sio chanzo cha taharuki mjini humo.

Taharuki mjini humo inasababishwa na wanyama pori.

Yamkini wenyeji wa mji huo wameombwa kukaaa majumbani mwao baada ya wanyama waliohifadhiwa katika hifadhi moja katikati ya mji huo kusombwa na mafuriko.

Wanyama waliotoweka ni pamoja na chui simba wa mwituni,dubu na hata mbwa mwitu.

Kati ya wale waliouawa watatu walipatikana ndani ya hifadhi hiyo ya wanyama.