Sherehe ya nyama ya mbwa
Huwezi kusikiliza tena

Sherehe za nyama ya mbwa zaanza Uchina

Sherehe ya kula nyama ya mbwa kusini magharibi mwa China imeanza huku kukiwa na pingamizi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wanyama. Takriban mbwa 10,000 watachinjwa na nyama yao kuliwa katika sherehe hizo zitakazofanyika katika eneo la Yulin mkoa wa Guangxi siku ya jumapili na jumatatu ili kuadhimisha kuanza kwa msimu wa joto kulingana na vyombo vya habari vya kitaifa.