Wasichana wa Chibok washinikizwa kuua
Huwezi kusikiliza tena

Wasichana wa Chibok washinikizwa kuua

Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC limeelezwa kuwa baadhi ya wasichana waliotekwa na wanamgambo mjini Chibok Nigeria wamekuwa wakishinikizwa kuwaua Wakristo.

Wanawake watatu ambao wanasema walikuwa wakishikiliwa katika kambi moja na wasichana hao wanasema wapiganaji wa Boko Haram waliwafunga mikono wanaume wa Kikristo.

Wasichana hao waliwachinja wanaume hao kwa kuwakata shingo.

Wanawake hao wanasema baadhi ya wasichana hao wa Chibok walikuwa na silaha.

Baadhi ya wasichana waliwachapa mateka wengine wa kike.