Maafisa wa kijeshi Indonesia, wanasema  takriban watu 100 wameuawa katika ajali mbaya ya ndege ya uchukuzi ya kijeshi huko Sumatra
Huwezi kusikiliza tena

Ndege ya kijeshi yaua ''100'' Indonesia

Takriban watu 100 wameuawa baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka mapema leo katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.

Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa tayari miili 49 imepatikana katika eneo la ajali.

Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.

Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules 130 ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 113 ilipoanguka.