Lupita Nyong'o:ateuliwa balozi wa kulinda Tembo
Huwezi kusikiliza tena

Lupita Nyong'o:ateuliwa balozi wa kulinda Tembo

Lupita Nyong'o wa Kenya ametoka mbali tangu alipopata tuzo ya Oscar ya mchezaji filamu bora msaidizi wa filamu ya mwaka 2013 iitwayo ''Twelve Years a Slave''.

Uso wake umetawala kwenye ukurasa mbalimbali wa mwanzo wa majarida ya urembo,

ambapo amepata sifa tele kwa kipaji chake na mitindo pia.

Sasa Jambo ambalo wengi hawakujua ni kwamba alianza kuwa mwanaharakati tangu utotoni, na hapa alikuwa akiimba kupambana na mauaji haramu ya tembo.