Viongozi mahasimu  wa Sudan Kusini Salva Kiir na Riek Machar
Huwezi kusikiliza tena

Riek Machar amuonya Salva Kiir

Daktari Riek Machar, aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan Kusini kabla ya kumeguka sehemu ya jeshini na kuanza uasi kupingana na rais Salva Kiir ameapa kuwa rais Kiir asipojiuzulu ataanzisha harakati za kuipindua serikali yake.

Tangazo hilo la Riek Machar limefanywa wakati ambapo wananchi wa Sudan Kusini wanasherehekea mwaka wa nne tangu wajinyakulie Uhuru kutoka kwa Sudan ya Khartoum.

Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda alizungumza na mtaalamu wa Maswala ya Sudan Kusini Mohammed Jaffar:na kwanza alimuuliza juu ya Tangazo la Dokta Riek Machar la kutaka kumtimua mamlakani Salva Kiir linaashiria nini Sudan Kusini.