Masharti ya mkopo uliopewa Ugiriki
Huwezi kusikiliza tena

Video:Masharti ya mkopo uliopewa Ugiriki

Kufuatia makubaliano mapya ya mkopo,Ugiriki italazimika kuimarisha utozwaji kodi,kupunguza malipo ya uzeeni na kutekeleza mabadiliko katika sera za wafanyikazi.

Aidha taifa hilo litalazimika kuwajibikia madeni iliyochukua na kuhakikisha imeweka mikakati dhabiti ya kuyalipa.

Iwapo itatekeleza mabadiliko hayo, Ugiriki itapokea Euro bilioni 95 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras ana matumaini kuwa makubaliano yaliyoafikiwa yataokoa mabenki nchini humo yasiporomoke.

Aidha bwana Tsipras amekiri kuwa sasa ni wakati wa kufanya maamuzi magumu ya sera za Ugiriki.