Nyuklia:Iran yakubaliana na mataifa 6 makubwa
Huwezi kusikiliza tena

Nyuklia:Iran yakubaliana na mataifa 6 makubwa

Makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yametangazwa rasmi baada ya majadiliano ya miaka mingi.

Makubaliano hayo yanaruhusu kuondolewa vikwazi vya kimataifa dhidi ya Iran ili kwa upande mwingine hatua za kuizuia nchi hiyo kuunda silaha ya nyuklia ziidhinishwe.

Makubaliano hayo kati ya Tehran na nchi nyengine sita zenye nguvu duniani yamefikiwa baada ya wiki kadhaa za majadiliano makali.

Katika mkutano wa waandishi habari huko Vienna mkuu wa sera za nje wa Umoja wa laya, Federica Mogherini amesema makubaliano hayo yanadhihirisha uwajibikaji wa pamoja kwa amani na kuifanya dunia kuwa salama.