Daktari John Magufuli
Huwezi kusikiliza tena

Uchaguzi wa Magufuli wazua hisia tofauti TZ

Kuchaguliwa kwa Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania Daktari John Magufuli kubeba bendera ya chama tawala cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu kumepokelewa na hisia tofauti na wananchi nchini humo. Ametumikia awamu tatu za uongozi akiwa waziri. Daktari Magufuli alichaguliwa mwishoni mwa wiki na mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma baada ya kuwashinda washindani wake Balozi Amina Salum Ali na Daktari Asha Rose Migiro. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Mapinduzi, Daktari Magufuli atakuwa na mgombea mwenza mwanamke Samia Suluhu. Sammy Awami anaripoti zaidi kutoka Dodoma.