Huwezi kusikiliza tena

BBC yafichua usafirishaji watoto

BBC imepata ushahidi unao onesha namna wachezaji wa hadi umri wa miaka kumi na nne wanasafirishwa kinyume cha sheria kutoka bara Afrika na Asia kinyume na sheria za FIFA.

shirika moja liliso la kiserikali limesema kuwa takriban vijana elfu kumi na tano wanasafirishwa kimagendo kutoka Afrika Magharibi kila mwaka.

Uvunjaji huu wa sheria za FIFA na kuwanunua wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18 kinyume cha sheria umeisababishia klabu ya Barcelona marufuku ya miezi kumi na nne ya ya kuhamisha wachezaji wake.

Barcelona ndio wanaoshikilia taji la klabu bingwa barani Ulaya. lakini hizo ni siasa za juu zaidi katika mchezo huo duniani, tofauti kabisa na hali ilivyo katika ngazi za chini.

Mwandishi wa BBC Piers Edwards anaeleza kutoka Liberia ikisimuliwa na John Solombi