Uchaguzi wa urais nchini Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Uchaguzi wa urais nchini Burundi

Gruneti limelipuka katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi wa urais.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema bomu hilo lililipuka katikati mwa mji karibu na medani ya Uhuru.

Gari moja liliharibiwa na hakuna aliyejeruhiwa.

Upinzani umetoa wito watu kutopiga kura.

Uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula mwingine umeitumbukiza Burundi katika vurugu.

Nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wa Rais hapo kesho.

Mwandishi wetu Salim Kikeke anaarifu zaidi kutoka Bujumbura.