Utabibu wa kiafrika ni halali ama haramu ?
Huwezi kusikiliza tena

Utabibu wa kiafrika ni halali ama haramu ?

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,waganga wa jadi maarufu kama 'wafumu' wanalaumiwa kuwa waongo na walaghai katika jamii.

Hata hivyo katika miji mbali mbali ya mashariki mwa nchi hiyo waganga hao wanajipigia debe na kuuza biashara yao kwa jamii.

Miongoni mwa dawa zinazo wavutia watu ni kama vile dawa ya kutibu ukimwi,saratani na dawa yakupata ujauzito kwa wanawake.

Baadhi ya watu husema dawa hizo ni za uongo nakutaka serikali iwachukulie hatua kali.

Mwandishi wa BBC BYOBE MALENGA alitembelea mji wa Baraka na kutuandalia taarifa ifuatayo.