Huwezi kusikiliza tena

Bibi wa Obama amtaka mjukuu wake, Kogelo

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umesema Rais Barack Obama hatatembelea kijiji alichozaliwa baba yake, wakati wa ziara yake.

Taarifa zilizotolewa na ubalozi huo zimesema hakuna mpango wa Rais Obama kutembelea Kogelo, kijiji alikozaliwa babake Obama Snr.

Zimebaki siku mbili tu kwa Rais huyo wa Marekani kuwasili Kenya kwa ziara rasmi ya kufungua mkutano wa kimataifa wa uekezaji.

Hata hivyo kuna baadhi ambao hawajakata tamaa, akiwemo bibi yake Mama Sarah Obama.

Sikiliza mahojiano kati ya Muliro Telewawa BBC na Mama Sara Obama.