Uhusiano baina ya raia wa Kenya na Marekani
Huwezi kusikiliza tena

Uhusiano baina ya raia wa Kenya na Marekani

Wakati rais wa Marekani Barack Obama anaitembelea Kenya ambapo wengi wanamfahamu kuwa na nasaba na Kenya kufuatia baba yake kuwa mzaliwa wa Kenya, Lakini huenda usifahamu kuwa kuna wa Marekani wengine nao wanahisi kuwa na uhusiano na nchi ya Kenya.

Hii ni kufuatia Rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta, alivyochochea hamasa kwa jamii ya wamarekani weusi nchini Marekani .

Mwaka 1968 wakazi wa mji wa East Palo Alto huko California walijaribu kubadilisha hata jina la mji wao uitwe 'Nairobi' kuenzi mji mkuu wa Kenya.

Japo baadae walishindwa kwa kura.

Mwandishi wa habari Dickens Olewe alikutana na viongozi wa vuguvugu la Nairobi huko Marekani na kutuandalia taarifa hii inasiyomuliwa na Dinah Gahamanyi