Huwezi kusikiliza tena

Yatima asiyesoma na kipaji cha Hesabu

Sikiliza ripoti ya Leonard mubali kuhusiana na msichana Anna Jackson kutoka Mtwara kusini mwa Tanzania.

Licha ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa tangu udogo na kusababisha kukatisha masomo yake, ameibuka na kuwa na kipaji cha ajabu, kwa kuwa na uwezo wa kutoa majibu ya hesabu yoyote ile ndani ya sekunde chache bila kuandika wala kutafakari kwa muda mrefu.

Japo kuwa ni miaka mingi sasa tangu aache masomo yake kutokana na maradhi hayo na uyatima, anasema akipata msaada anaweza kusoma ama kuajiriwa kazi za kutunza hesabu licha ya kutokuwa na mafunzo yoyote.