Huwezi kusikiliza tena

Obama kuhutubia katika Umoja wa Afrika.

Rais Barack Obama leo anatarajia kuwahutubia viongozi wa Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Anatarajiwa pia kugusia pamoja na mambo mengine, masuala ya demokrasia na utawala bora.

Halima Nyanza amezungumza na Mchambuzi wa mambo Said Msonga na kumuuliza je anadhani viongozi wa Afrika ambao baadhi yao wamekuwa wakilalamikiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, kutokuwa na utawala bora pamoja na demokrasia katika nchi zao, wataweza kumsikiliza Rais Obama?