Waganda wapewa vibali vya kufanya kazi nchini Saudia
Huwezi kusikiliza tena

Waganda wapata vibali vya kazi Saudia

Mazungumzo yaliyofanywa kati ya Uganda na Saud Arabia, yametoa nafasi kwa raia wa Uganda kupata vibali vya kufanya kazi nchini humo.

Hata hivyo kuna wasiwasi huenda Waganda hao wakanyanyaswa.

Hali hii inakuja wakati kuna malalamiko ya wanawake wanaokwenda kufanya kazi katika nchi za mashariki ya kati kunyanyaswa.

Muruli Mukasa ni Waziri wa Jinsia na maendeleo ya jamii wa Uganda.