Huwezi kusikiliza tena

Mchezo wa Riadha watiwa dosari Kenya

Ripoti zinadai Kenya na Urusi ni miongoni mwa nchi ambazo wanaraidha wake hutumia dawa za kusisimua misuli katika michezo ya Olimpiki. Ripoti hiyo pia imeeleza kwamba theluthi moja ya nishani katika mashindano hayo kati ya mwaka 2001 na 2012 zinatokana na wanariadha wake kutumia dawa hizo.

Mwandishi wa BBC, Lizzy Masinga alizungumza na mwanaraidha wa Kenya ambaye ni bingwa mara tatu wa mbio za mita 3000 za kuruka viunzi, Moses Kiptanui...na kutaka kujua maoni yake kuhusu tuhuma hizo