bajaji zenye misemo
Huwezi kusikiliza tena

Misemo ya bajaji Tanzania

Pikipiki za matairi matatu ama maarufu kwa jina la bajaji nchini Tanzania, zimekuwa ndio usafiri mkubwa mbadala wa umma katika jiji la Dar es Salaam. Kwa upande mwingine, pikipiki hizi zimekuwa njia mbadala ya kusambaza ujumbe mbalimbali kwa watu. Tangu zianze kuhudumia abiria miaka michache iliyopita nchini humo, maneno na misemo yenye bashasha na ya kufurahisha, yamekuwa ndio mtindo wa kileo. Zamani maneno haya ungeyakuta kwenye kanga, kawa au kipepeo tu. Lakini siku hizi unayakuta yameandikwa pia nyuma ya pikipiki hizi na kugeuka burudani kubwa miongoni mwa watumia barabara. Mwandishi wa BBC Sammy Awami amefuatilia misemo hiiā€¦..