Huwezi kusikiliza tena

Kanda za sauti ya Osama zasikika

Osama bin Laden,alikuwa ni kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda. Katika harakati za kumsaka kufuatia mashambulizi ya September 11 Marekani,mnamo mwaka wa 2002,wanajeshi walivamia yaliyokuwa makao yake huko Kandahar, Afganistan. Miongoni mwa vitu vilivyopatikana ni zaidi ya kanda 1500 za kwake. BBC imepata fursa ya kipekee kuzisikiliza kanda hizo ambazo zimetafsiriwa na proffesa Flagg Miller kutoka chuo kikuu cha Carlifornia.

Mwandishi wa maswala ya usalama wa BBC Gordon Corera amezungumza na proff Miller kuhusu kanda hizo na kumuuliza zinadokeza nini kuhusu kundi la Al Queda. Taarifa yake imetafsiriwa na kusomwa studio.