Huwezi kusikiliza tena

Usafiri wa magari changamoto Nigeria

Afrika inafahamika kwa kuwa na miji yenye misongamano mikubwa ya magari duniani na matukio mengi ya ajali za barabarani zinazosababisha vifo.

kwa mujibu wa Benki ya dunia, watu zaidi watapoteza maisha kutokana na ajali za barabarani barani Afrika kuliko idadi ya Watu watakaopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030, hivyo wiki hii tutaangalia hali ya barabara barani Afrika na miundombinu duni.

Sam Olukoya anaangazia hali ilivyo jijini Lagos, Taarifa yake inasimuliwa na Gladys Njoroge.