Mwanaharakati wa Kijamii nchini Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Wakenya wengi wazuiliwa magereza Ngambo

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Kenya wametoa wito kwa serikali kuhakikishia haki kwa washukiwa wanaozuiliwa katika mataifa ya kigeni.

Baadhi ya Wakenya hao walio nchi za kigeni wanashutumiwa kuhusika na vitendo vya kitapeli na ugaidi.

Kwa mujibu wa ripoti mamia ya Wakenya wanazuiliwa katika magereza ya ughaibuni kwa mashtaka ya aina mbali mbali. Mkutano ambao unajumuisha ma mia ya raia wa Kenya, kutoka mashirika ya kutetea haki za kibinadamu, wanasiasa na familia za wale walio katika magereza ya ngambo wameitaka serikali, kushinikiza washukiwa hao kufikishwa mahakamani au kuachiliwa huru.

David Wafula Anaripoti kutoka Nairobi